Latest Updates

Kisa kilichomkuta jamaa wakati wa jaribio la kuiba hela kwenye ATM, tazama video hapa

Siku za mwizi ni arobaini, huyu zake zilifika hivi.
Jamaa mmoja Australia alifika katika ATM lengo lake likiwa ni kuiba, akategesha kitu ambacho ni kama baruti hivi ili mashine ilipuke aibe pesa.
Mpango wake ulikwama, ulitokea mlipuko mkubwa kwenye ATM ambao ulimtupa mbali, akainuka na kukimbia huku mashine ya ATM ikiwa imeharibika vibaya kutokana na mlipuko huo.
Polisi wa Jiji la Darwin, Australia ilikotokea tukio hilo wanahisi jamaa huyu anahusika na tukio la namna hiyo ambalo lililotokea siku ya Sikukuu ya Christmas.
Kuna video ya sekunde hamsini ikionyesha tukio zima, itazame hapa.
                               

0 Response to "Kisa kilichomkuta jamaa wakati wa jaribio la kuiba hela kwenye ATM, tazama video hapa"

Post a Comment