Latest Updates

Eti Kanye West anawafunika mastar wengine wa kiume kwa mavazi?

Kumekuwa na mashindano ya ubunifu wa mitindo mbalimbali ya mavazi, wakati mwingine tumeona mastaa ambao hubuni mavazi yao wenyewe, hivi ukiambiwa umchague staa wa kiume ambaye ameongoza kwa kuvaa vizuri zaidi utamchagua nani? Nilishawahi kusikia watu wakisema eti jamaa hajui kupangilia mavazi, ana mtindo wa kuvaa ambao hauvutii na ukimuangalia unaona kwamba ni kama hajali kuhusu mavazi yake. Jarida la GQ wamefanya tafiti zao na watu wamepiga kura, majibu yemeonyesha kuwa rappa Kanye West, ndiye bingwa wa kutupia swaga kwa mwaka 2014. Jamaa waliofanya tafiti wamesema mavazi ya Kanye West yametafsiri na kubadili mazingira ya fashion kwa wanaume wengi, mavazi yake ni kama yamekuwa yakielezea kesho zaidi kwenye Dunia ya mitindo. Kwenye utafiti huu, Kanye kawashinda mastaa wengi ikiwemo staa wa movie ya ‘Long Walk to Freedom‘ , Idris Elba. Je unakubaliana na tathimini za Jarida la GQ kuwa Kanye West ndio ameleta mapinduzi katika mtindo wa uvaaji kwa wanaume 2014?

0 Response to "Eti Kanye West anawafunika mastar wengine wa kiume kwa mavazi?"

Post a Comment