Latest Updates

MAZISHI YA MMILIKI WA LINA'S CLUB BUKOBA


    

Wananchi wakiwa barabarani kushuhudia msafara huo ukipita. “Msafara ulianzia mochwari ya Hospitali ya Bukoba, ukapita katika klabu yake ya Lina’s kisha ukapitia mtaa wa Jamhuri lilipo Soko Kuu la Bukoba kisha kuelekea kijiji cha Kyaikailabwa. 

“Ilikuwa si mchezo, hii ni HISTORIA kwa Bukoba. Haijawahi kutokea msiba wa mtu wa kawaida ukawasababisha watu kujipanga barabarani, trafiki kuongoza harakati utafikiri mapokezi ya rais,” kilisema chanzo. 

Inadaiwa kuwa msafara wa magari ulivunja rekodi kwani wakati magari mengine yalikuwa yameshafika makaburini, mengine yalikuwa bado kwenye foleni nyumbani. 


Chanzo hicho kilizidi kupasha habari kuwa, msafara wa kutoka nyumbani kwa marehemu, Bukoba mjini hadi katika Kijiji cha Kyaikalabwa ambacho kipo umbali wa kilomita 3, ulikuwa mrefu kiasi ambacho magari yalijipanga kuanzia mjini hadi kaburini. 

“Palifunga kabisa, huwezi amini ule msururu wa magari ulianzia Bukoba mjini hadi Kyaikailabwa, magari yenyewe asilimia kubwa yalikuwa ya maana.“Marehemu alikuwa tajiri na baadhi ya marafiki zake pia walikuwa matajiri sasa ilikuwa ni balaa maana magari ya kifahari tupu yalipamba msafara huo. 

                                          WAKATOLIKI WAKATAA KUMZIKA
Chanzo hicho makini kilidai kuwa, kutokana na mazingira ya kifo na watu waliokwenda kuomba misa ya msiba huo kutokidhi vigezo, viongozi wa kanisa katoliki walikataa kuongoza ibada ya mazishi.
Ilidaiwa kuwa waliokwenda kuomba misa hiyo hawakuwa na sifa za kiimani (hawakuwa wakatoliki) sambamba na kutotumia busara wakati wa kujieleza.


Ndugu wa marehemu wakilia kwa uchungu. “Waliokwenda kuomba misa hawakuwa wakatoliki halafu mbaya zaidi hawakuwa na busara wakati wa kujieleza, mapadri wakawagomea kuongoza ibada hiyo,” kilisema chanzo.
Badala yake, inadaiwa kuwa ibada ya kumuombea marehemu iliendeshwa na wakristo wa Kilokole iliyofanyika nyumbani kwake. 

TUJIKUMBUSHE
Marehemu Mtensa aliyeacha mjane na watoto kwa mkewe wa ndoa, alikutwa na umauti Novemba 18, mwaka huu saa chache baada ya kuzidiwa akiwa ndani ya gari LAKE akifanya mapenzi na mchepuko wake aliyejulikana kwa jina la Jackline Hassan.


Mwili wa marehemu ukiingizwa kaburini. Kitendawili kingine kilichoteguliwa ni kuhusu msichana JACK, mwenye umri wa miaka 25, ambaye awali iliaminika kuwa ni mpenzi wake aliyekutana naye ghafla tu, lakini inasemekana alikuwa ni mpenzi wa muda mrefu wa Mtensa na kwamba hata wakati flani alipokuwa akienda Uganda kuwaangalia watoto wake waliokuwa wakisoma huko, alikuwa akiongozana naye. 

Aidha, STORI nyingine kutoka huko zinadai kwamba polisi wamekuwa wakitaka kumuachia msichana huyo wakiamini hakuwa na kosa, ingawa hakuna taarifa zozote zilizokwishatolewa hadi sasa kuhusu uchunguzi waliofanya.

0 Response to "MAZISHI YA MMILIKI WA LINA'S CLUB BUKOBA"

Post a Comment