Kwa mujibu wa madai hayo, inasemekana kwamba Gardner amekimbilia mahakamani akidai apewe talaka na waweze kugawana mali walizochuma wote ili kila mmoja achukue hamsini zake.
"Msinitaje jina ila ninachowaambia ni kwamba Gardner tayari ameshampata mwanasheria anataka kumshitaki Jaydee, anachohitaji ni kugawana mali zao, kila mtu afanye maisha yake na ukiangalia tu Gardner hana mpango tena wa kuendelea na maisha ya ndoa na Jaydee ila Jide yeye anaamini bado anamatumaini ya kurudiana wawe pamoja na hasa kinachomuuma ni kugawana mali" kilisema Chanjo hicho.
0 Response to "GARDNER AKIMBILIA MAHAKAMANI KUNUSURU MGAO WA MALI WALIZOCHUMA NA JAYDEE"
Post a Comment