Latest Updates

BABY MADAHA NA INSPECTOR HAROUN WANASWA KIMAHABA


Katika hali ya kushangaza, mastaa wawili wa muziki, BABY Madaha na Haroun Kahena ‘Inspector Haroun’ wamenaswa usiku wakila bata huku wakiwa kimahaba.

Tukio hilo lilinaswa na KAMERA ya paparazi wetu hivi karibuni kwenye pub moja iliyopo maeneo ya Kijitonyama jijini Dar ambapo awali Inspector alionekana akiwa amemkalia Madaha huku wakipigana mabusu.

Baada ya paparazi wetu kujitokeza na kuanza kuwafotoa, Inspector ambaye ni mume wa mtu alishituka na kujinasua kutoka kwenye mwili wa mwanadada huyo.Alipoulizwa juu ya kile alichokuwa akifanya wakati ni mume wa mtu, Inspector alisema:

“Kaka kwani kuna kibaya gani tulichokuwa tunafanya, tupo hapa tunapanga mambo yetu ya muziki na wala hakuna ishu zaidi.”BABY Madaha kwa sasa haijulikani anatoka kimapenzi na nani ila Inspector Haroun ni mume wa Bahati ambaye alifunga naye ndoa mwaka 2004 na wamejaaliwa kupata watoto wawili ambao ni Nassir na Shadya.

0 Response to "BABY MADAHA NA INSPECTOR HAROUN WANASWA KIMAHABA"

Post a Comment