Latest Updates

ALICHOKISEMA QUEEN DARLEEN KUHUSU SIKU YAKE YA KUZALIWA

                      
Siku ya leo msanii Queen Darleen anasherehekea siku yake ya kuzaliwa, tumebahatika kufanya nae mahojiano na tumemuuliza ni vitu gani hua 
anafanya siku kama ya leo na Queen alisema ” Siku kama ya leo inapofika saa 6 (Usiku) kama mwili wangu haupo msafi basi natia udhu kisha naanza sala na kumuomba mwenyezi Mungu kwa sababu kuna kuugua na 
pia
 kuna kufakwa najaribu kumuomba mwenyezi Mungu anisaidie uhai mrefu”
Alipoulizwa kuhusu kama atafanya sherehe, Queen Darleen alisema ” Sijawahi kufanya sherehe

mimi kama mimi lakini leo marafiki zangu wakina Mwasiti, Almasi, K Star Diamond kina shilole wote wameamua kunifanyia kitu hapa nyumbani kwangu kuanzia saa 2 usiku, mi sijui ni kitu gani watanifanyia. Kwa hiyo suprise lakini nimesema sitaki zawadi ya gari, nimeshampa warning kabisa Diamond”

0 Response to "ALICHOKISEMA QUEEN DARLEEN KUHUSU SIKU YAKE YA KUZALIWA "

Post a Comment