
Melissa mwenye umri wa miaka 46 amepanga kumshitaki Dr Gwen Korovin ambaye alidaiwa kutokuwa na kibali cha kufanya kazi za utabibu katika Yorkville Endoscopy Clinic huko Manhattan ambapo Joan Rivers alifariki akiwa na umri wa miaka 88.
Rafiki wa karibu wa Melissa ameiambia MailOnline kuwa Melissa yuko serious na mpango huo.
Amesema ingawa ni vigumu sana kujadili nae kitu kinachomuudhi wakati huu, lakini ataanzisha mashtaka hivi karibuni.
Taarifa zimeeleza kuwa daktari huyo licha ya kutokuwa na kibali bado anaendelea kutoa matibabu katika hospitali hiyo wakati ambapo bado anachunguzwa na vitengo vya usalama vya Marekani.
0 Response to " DAKTARI ASHTAKIWA KWA KUSABABISHA KIFO CHA MUIGIZAJI MAARUFU"
Post a Comment