Latest Updates

Picha: Mpiga picha anaeiwakilisha Tanzania katika Big Brother Africa 2014, Muigizaji huyu wa kike anaweza kutajwa pia


Waandaaji wa shindano la Big Brother Africa wameendelea kutangaza majina ya washiriki wa shindano hilo, na leo wametaja majina ya washiriki watatu akiwemo Idris kutoka Tanzania.

Kwa mujibu wa mtandao wa Big Brothe Africa, Idris Sultani ameeleza kuwa ana mikakati na anatumaini  washiriki wenzake watamgeukia yeye pale wanapotaka kuwa inspired au wanapokuwa katika wakati mgumu.
Hata hivyo, taarifa za awali ambazo hazijathibitishwa bado na waandaaji wa Big Brother zilimtaja Idris Sultani na muigizaji Irene Veda kuwa ndio watakaoiwakilisha Tanzania.
Baada ya Idris kutangazwa leo, taarifa hizo za awali zimepewa nafasi zaidi. huenda Irine akatangazwa hivi karibuni japo hakuna uhakika wa kutosha.
Washiriki wengine waliotajwa leo kuwa kati ya wanaowania ushindi katika shindano hilo lilopewa jina la ‘Hot Shots’ ni Goitse kutoka Uganda na Esther kutoka Uganda.
 

0 Response to " Picha: Mpiga picha anaeiwakilisha Tanzania katika Big Brother Africa 2014, Muigizaji huyu wa kike anaweza kutajwa pia"

Post a Comment