Latest Updates

Meninah: Mapenzi yatavuruga muziki wake


Mwimbaji wa Bongo Flava aliyewahi kuwa mshiriki wa BSS, Meninah  amesema anaogopa kuwa katika uhusiano wa mapenzi hivi sasa kwa kuwa anaamini mapenzi yatavuruga muziki wake.
Akiongea katika kipindi cha Hatua Tatu cha 100.5 Times Fm, Meninah ameeleza kuwa hivi sasa yuko single na hajawa na mpango wa kuingia katika uhusiano kutokana na sababu hizo.
Meninah akiwa studio na Maryam Kitosi (100.5 Times FM)
“Kwa sasa niko Single naangalia kazi yangu kwanza... Nikiingia kwenye mahusiano kazi yangu itakuwa shaghala bagala.” Amesema Meninah.
Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kuwa mwimbaji huyo ana ukaribu na Diamond lakini alikanusha na kueleza kuwa hajawahi hata kuwa na ukaribu na mkali huyo.
Unaweza kuwa umeshasikia na unaamini Meninah yuko kwenye uhusiano na….. Lakini msikilize pia yeye. “Unajua watu wanaamini ukiwa msichana mzuri basi ni lazima uwe katika uhusiano!”
Meninah ameachia wimbo mpya unaoitwa ‘Pipi ya Kijiti’

0 Response to "Meninah: Mapenzi yatavuruga muziki wake"

Post a Comment