Latest Updates

Chris Brown yuko hatarini, Majirani wapya watishia kumpiga risasi


Mwimbaji wa Loyal, Chris Brown ambaye alitoka jela hivi karibuni na kuamua kutafuta amani kwa kuhama nyumba aliyokuwa akiishi kukwepa ugomvi na majirani zake ni kama ameruka majivu na kukanyaga moto.
Kwa mujibu wa TMZ, mwimbaji huyo aliamua kuuza nyumba yake ya kifahari iliyokuwa Hollywood Hills kufuatia ugomvi wa kila siku na majirani zake waliomfikisha kwenye vyombo vya sheria mara kadhaa kwa madai ya kuwanyima raha na familia zao kwa vitendo vyake. Baada ya kuuza nyumba hiyo alinunua nyumba mpya, California.
Kwa bahati mbaya majirani wapya wa mwimbaji huyo wanaonekana kuwa na maamuzi magumu zaidi ya wale wa awali waliokuwa wanampeleka kwenye vyombo vya sheria.
Akiongea na TMZ, jirani mmoja alieleza kutofurahishwa kwake na ujio wa Chris Brown kwenye ujirani wao na kuahidi kuwa endapo atagusa nyumbani kwake atampiga risasi.
“It can be the devil. I can care less.. I don’t care if they are having orgies. It can even be Sadam Hussein for all I care, as long as he doesn’t trespass onto my property. If he does, I shoot him.”
Jumba jipya la Chris Brown lina vitu vya kifahari kama uwanja wa kuchezea tennis, dance studio, club house, commercial ice cream bar na mengine mengi huku eneo zima likuwa na ukubwa wa eneo la mraba futi 8,000 na vyumba sita vya kulala.

0 Response to "Chris Brown yuko hatarini, Majirani wapya watishia kumpiga risasi"

Post a Comment