Taarifa zilizotufikia hivi punde kutoka kwa chanzo cha kuaminika zinaeleza kuwa muigizaji mkongwe Mzee Small ambaye jina lake halisi ni Saidi Ngamba amefariki dunia katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.
Mzee Small alikuwa mgonjwa kwa muda mrefu na aliwahi kueleza kuwa aligundulika kuwa ana tatizo la damu kuganda kichwani lakini pia ugonjwa uliompelekea kulemaa mkono.
Taarifa zinaeleza kuwa Mzee Small alizidiwa kwa ugonjwa wa presha hali iliyompelekea kufikwa na umauti.
Tutaendelea kukujuza kuhusu msiba huu uliukumba tasnia ya filamu na watanzania wote wazalendo wanaukumbuka mchango wa Mzee Small katika uigizaji na ucheshi.
Apumzike kwa Amani.
0 Response to "Tanzia: Mzee Small afariki dunia"
Post a Comment