Latest Updates

RICK ROSS MATATANI, ATISHIWA MAISHA NA WATU WASIOJULIKANARAPA ambaye pia ni boss wa MMG, Rick Ross ametishiwa maisha na watu zaidi ya 100 waliomuwekea kizuizi njiani wakati akielekea kwenye tamasha la Summer Jamz lililoandaliwa na kituo cha radio cha HOT 107.5 huko Detroit.

Umati wa mashabiki waliokuwa wanamsubiri kwa hamu Rozay kupanda jukwaani walishitushwa na taarifa zilizotangazwa na Jay Hicks ambaye ni muongozaji wa vipindi wa kituo hicho kuwa Rick Ross amehofia maisha yake na ameshindwa kufika ingawa yuko karibu na tamasha hilo.

“Majira ya tano, wakati anasokea kuja hapa Chene Park, amekutana na watu 100 hapo nje. Tumejaribu kufanya kila tuwezalo na kumuomba arudi. Anahofia maisha yake.” Alisema Jay Hicks.

Rick Ross amewahi kukutana na vitisho mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushambuliwa kwa risasi japo hazikumgusa.

0 Response to " RICK ROSS MATATANI, ATISHIWA MAISHA NA WATU WASIOJULIKANA"

Post a Comment