Latest Updates

Bibi wa miaka 65 mwenye uwezo mkubwa wa kucheza sarakasi apigwa marufuku


Bibi mmoja wa mwenye umri wa miaka 6, Dianne ‘DD’ Barker ambae anaonekana bado yuko fit na ana uwezo wa kuruka sarakasi kwa manjonjo amepigwa marufuku na serikali za mtiaa huko Ohio, Marekani.
Bibi huyo alitumiwa barua na mwanasheria wa Maricopa Association of Government (MAG) ikimtaka kusitisha zoezi la kufanya maonesho ya sarakasi ana ya ‘cartwheels’ hadharani mara moja.
Mwanasheria huyo alifafanua kuwa wameamua kusitisha zoezi lake kwa kuwa ni kinyume cha sheria na kwamba wanafanya hivyo kuzuia aina hiyo ya mchezo anaocheza hadharani ili kuzuia uwezekano wa kupata majeraha na matatizo mengine ya afya kwa kuwa yeye sio mtaalam wa mambo hayo bali anacheza tu kwa uwezo binafsi.
Bi Baker alipinga vikali hatua hiyo na kudai kuwa anaonewa na kwamba hata barua ya mwanasheria huyo ilijaa vitisho dhidi yake na kueleza kuwa yeye haoni tatizo kati ya kuwa mtaalam na kuwa na uwezo.
Mwisho wa siku bibi huyo ameamua kukubali kuchana na sarakasi za cartweels japo amesema anajiandaa kutoka kivingine.

0 Response to "Bibi wa miaka 65 mwenye uwezo mkubwa wa kucheza sarakasi apigwa marufuku"

Post a Comment