Latest Updates

WEMA AWAFUNGA MIDOMO WABAYA WAKE


BAADA ya msanii wa filamu nchini Wema Sepetu kuibuka kuwa mshindi wa shindano la Ijumaa Sexiest Girl mapya yaibuka huku baadhi ya wadau wakihusisha ushindi huo pamoja na fujo zilizowahi kuripotiwa kufanywa na msanii huyo katikia ofisi za Global Publish.

Wema aliibuka mshindi wa Sexiest Girl zambapo shindano hilo liliandaliwa na Global Publish huku msanii huyo akiwa amewabwaga wenzake akiwemo Jokate, Wolpa pamoja na Lulu.

Baadhi ya watu mbalimbali wamehusisha ushindi huo na fujo ambazo mwanadada huyo aliwahi kuzifanya katika ofisi za Global ambazo ndizo zilizoandaa shindano hilo.

Kupitia ukurasa wake wa Inastagram Wema aliandika juu ya ushindi huo, huku akionesha kushangazwa na baadhi ya watu wanaoshangazwa kushinda tuzo hiyo huku wengine wakihusisha na fujo zilizowahi kutokea.

“ If u got it flaunt it, Ndo nishashinda kama hujapenda kasage chupa kunywa…. maana naona sasa its too much khaaaaaaaa….! Ebu mnitue mie mtoto wa watu… And again much love to y’all dat support me… nawapenda sana…. nimemaliza…. Award yangu ndo hiiiiiiiiooooooooo…… next year tusubiri mwingine…. nalala zangu…. tukutane kesho…. najua wengi mnanipenda ni wachache wenye vijiba vyao vya roho…. Wema atabaki kuwa Wema tu… Bhaaaaas…

0 Response to "WEMA AWAFUNGA MIDOMO WABAYA WAKE"

Post a Comment