Jumamosi tangazo hilo linalosomeka hapa "TANGAZO" limeweza kubainisha internet explorer toleo la 6 hadi la 11 yote yameweza kugundulika yanatoa mwanya kwa wahalifu mtandao kupenya kwa watumiaji na kuchukua taarifa zozote zitakazo patikana kwenye computer zao.
Aidha, Kampuni inayo jihusisha na na maswala ya ulinzi mtandao ya "FireEye" imeonyesha takwimu yakua asilimia 56 ya vi vinjari kwa hadi ilipofikia mwaka 2013 vilikua hatarini kuingiliwa na wahalifu. na kubainisha kwamba wahalifu wamekua na uwezo wa kutengeneza vivinjari visivyo sahihi vinavyo weza ruhusu wahalifu hao kuingilia computer za watu mara tu watumiaji wa vi vinjari hivyo wanapo vitumia.
Microsofti imeshindwa kupata suluhu ya tatizo hilo ambapo CERT ya marekani imetoa tahadhari linalosomeka hapa "CERT ALERT" yakuwa watumiaji vivinjari vya "internet explorer" wanapaswa kubadil vivinjari kwa sasa na badala yake watumie vingine hadi hapo tatizo litakapo rekebishwa na kutangazwa vingenevyo.
Aidha,Christian Tripputi Ametumia muda huu kuonya watumiaji wa Window XP yakuwa kwa sasa wako hatarini kwani hakuna tena huduma zitakazo endelea kutolewa kwa Window hiyo na wahalifu mtandao wamesha anza kuleta madhara kwa wote wanaoendelea na matumizi ya windo hiyo na kusisistiza hapata kuwa na msaada kwa waathirika. Taarifa ya awali ilyotelewa na Yusuph kileo kuhusiana na matumizi ya Window XP inasomeka hapa
“TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA WINDOW XP"
0 Response to "TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA “INERNET EXPLORER” "
Post a Comment