Latest Updates

TUFURAHIE MAFANIKIO YA LUPITA


Siku zote katika maisha inapotokea mafanikio kwa mtu au jambo la ushindi, kila mmoja wetu hutumia muda wa kusifia tukio hilo huku na sisi tukitumia muda huo katika kuponda wale ambao tunahisi hawajafanya kitu katika tasnia ya filamu, hilo limekuja baada ya binti mzaliwa wa Mexico na raia wa kenya Lupita kujizolea tuzo za Oscar.Nimeona ujumbe mbalimbali katika mitandao ya kijamii kuna watu wametoa hisia zao, lakini kuna wakati ambao huwa tunashambuliana wenyewe kwa wenyewe bila kuangalia mwanzo wa tatizo letu la asili, ambalo ni kukosekana tuzo tu za ndani ambazo ndio kichocheo.


Lakini wakati tunaona yale ya Lupita Nyong’o mtoto wa Profesa na mazingira ambayo yalimfikisha hapo tunaangalia watoto wa wakulima kama Jackson Kabigiri ambaye hata shule yake alisoma hapa hapa hakupata mwanga zaidi kufika mbali na kusoma marekani aliposoma Lupita?
        

Asili ya mafanikio na kufika mbali pia uchangiwa na upendo, uelewa na fursa kwa mzazi, ambalo Lupita pamoja na baba yake kuwa mwanasiasa mkubwa bado hakuona sababu ya kumshawishi mwanaye ajiingize katika siasa ili wajenge familia ya kisiasa na kupokezana uongozi katika nyanja za kisiasa.


Ninaposema upendo maana yangu ni kwamba kama baadhi ya vijana ambao wamekuwa wakipigania tasnia hii ya filamu kwa muda mrefu nao wakafunguliwa na kuwa na mwanga na kubaini mambo yanavyokwenda ulimwenguni basi nao ingekuwa ni kitu cha kujivunia


Bongo tuna wasanii wengi sana ambao mfumo kwao umekuwa tatizo, niliamua kumuongelea Jackson Kabirigi kwa sababu ndiye msanii ambaye kwa mwaka 2013 kwa kiwango cha bongo aliweza kufika mbali hadi filamu kuibuka kama filamu bora ya kiasili.

         
Nilitegemea sana kuongelewa na kila chombo kama ni sehemu ya kutambua juhudi kidogo dogo zinazofanywa na wasanii wetu pamoja na kuwa na uwezo mdogo katika ushiriki wa matamasha ya kimataifa, pale kinapoonekana kidogo kitolewa ushabiki kama watu walivyoshabikia kwa Lupita.
          

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alikuwa bega kwa bega kumtia moyo Lupita kwani alikuwa akifuatilia mchakato wa tuzo hizo kwa kutuma ujumbe katika mitandao ya kijamii, lakini hapa kwetu pamoja na filamu ya mdundiko kurudi na ushindi sina hakika hata kama kuna kiongozi wa filamu alitoa pongezi kwa ushindi huo.

0 Response to " TUFURAHIE MAFANIKIO YA LUPITA"

Post a Comment