Latest Updates

SHILOLE AYAANIKA MAHUSIANO YAKE


HATIMAYE mwanadada ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Shilole ameamua kuweka wazi uhusiano wake wa kimapenzi na kudai kuwa yupo mbioni kufunga ndoa.
Msanii huyo ameweka wazi uhusiano wake huo wa kimapenzi na msanii mwenzie wa muziki wa kizazi kipya anayejulikana kwa jina la Nuhu Mziwanda ambapo amedai kuwa wapo teyari kufunga ndoa.
Wakizungumza katika kipindi cha XXL, Clouds Fm Shilole na Nuhu waliweka wazi hisia zao hizo za kimapenzi na kudai kuwa wamekuwa kwenye uhusiano huo kwa miezi mitatu sasa.
Nuhu alieleza kuwa wanajipanga ili mambo mengine yaweze kwenda sawa kwa ili vitu vingine viweze kufanyika ambapo alidai kuwa walikutana na Shilole studio Kijitonyama jijini Dar es Salaam, ambapo mwanadada huyo alienda hapo kwa ajili ya kazi ya kimuziki.
Kwa upande wake Shilole alidai kuwa hajaona sababu ya kuufisha uhusiano huo kwani kila mmoja anampenda mwenzie hivyo aliweka wazi kuwa yupo teyari kufunga ndoa.

0 Response to "SHILOLE AYAANIKA MAHUSIANO YAKE"

Post a Comment