
Rehema Saidi akielezea kitendo alichofanyiwa mtoto wake.
Newala. Kutokana na kumwamini
mumewe, Rehema Saidi, mkazi wa kijiji cha Rahaleo, Kata ya Mkunya Wilaya
ya Newala mkoani Mtwara, hakuwahi kutia shaka pale alipomwacha na
watoto, wakati yeye alipolazimika kutoka kwenda sehemu yoyote kwa ajili
ya shughuli za kifamilia.
Rehema na mumewe Juma Malolo
waliishi na watoto wawili; mwenye umri wa mwaka ambaye walimzaa pamoja
na mwenye umri wa miaka tisa ambaye (Rehema) alimzaa kwa mwanamume
mwingine kabla ya kuolewa mara ya pili.
Mwanamama huyu anasema aliishi
kwa raha mustarehe na familia yake na katika mazingira ya kawaida,
hakuwahi kuwaza kutokea kwa kitendo alichokishuhudia Agosti, 14 mwaka
jana, pale alipomkuta mumewe (Malolo) akimbaka binti yake (jina
tunalihifadhi).
Rehema anasimulia kwamba siku
ya tukio alikuwa akitoka sokoni alikokwenda kuchuuza mbogamboga kwa
ajili ya kupata fedha za kujikimu yeye na familia yake.
¡°Niliporudi nyumbani
nilifungua mlango bila hata ya kubisha hodi kwa sababu ni nyumbani
kwangu na wala sikuwa na hofu ya jambo lolote¡-sikuamini pale
nilipomkuta mume wangu akiwa anambaka mtoto wangu, kwanza nilipigwa na
butwaa, nikapandwa na hasira, nilimvamia na kuanza kumpiga Niliumia sana
kiasi siwezi hata kuhadithia aina ya maumivu niliyoyapata,¡± anasimulia
kwa huzuni.
Anabainisha kuwa baada ya
hapo, alitoka nyumbani hapo kuwaita majirani ili waweze kushuhudia
kitendo hicho, lakini aliporejea hakumkuta mumewe kwani alikuwa
ameondoka na kibaya zaidi alichukua fedha zilizotokana na biashara yake
Sh40,000 ambazo zilikuwa ndiyo akiba pekee aliyokuwa amebaki nayo.
¡°Nilikwenda kwa baba wa mtoto
kumwambia ili anisadie fedha ya kwenda mjini kutoa taarifa polisi
lakini alisema hana fedha. Hivyo nilishindwa kwenda na hata hospitali
kumpima, kwa sababu sikuwa na fedha tena ...nilibaki nyumbani huku
nikilalamika kwa kitendo alichofanyiwa mwanangu,¡± anasema Mariam.
Anaeleza kuwa alikaa siku tatu
bila kumwogesha binti yake kwa lengo la kutunza ushahidi wa kitendo
alichofanyiwa na wakati huo alikuwa akitafuta fedha ili aende polisi na
baadaye kumpeleka hospitali, lakini hakufanikiwa.
Mariam anasema baada ya siku
tatu kupita huku akiwa amepoteza matumaini ya kupata nauli, alimwogesha
mtoto huyo, hivyo ni dhahiri kwamba alipoteza ushahidi wa kitendo
alichofanyiwa.
Ilikuwaje?
Rehema anasema siku ya tukio,
Agosti 14 mwaka jana aliondoka nyumbani kwake saa 11 alfajiri kwenda
shambani kwa Mzee Makwedu umbali wa kilomita tatu kutoka kijijini kwake,
kununua majani ya kunde ili ayapeleke Mjini Newala kuyauza.
Anasema alimwacha mumewe na
watoto wawili. ¡°Nilimuaga mume wangu na kumwacha na watoto wote wawili,
kwa kuwa nilimwacha na mtoto mchanga wa mwaka mmoja niliamua kufanya
haraka ili asije akaanza kulia wakati sijarudi,¡± anasimulia na
kuongeza:
¡°Kwa hiyo nilikuwa nakimbia wakati wa kwenda na hata wakati wa kurudi, lakini nilichokiambulia ni hicho nilichokiona.
Anasema katika miaka miwili ya
ndoa aliyoishi na Malolo hakuwahi kuwa na shaka juu ya binti yake,
kwani alihakikisha anamtimizia mumewe mahitaji yote ya ndoa.
¡°Kama mwanadamu niliwahi
kuwaza kwamba mume wangu angeweza akawa na uhusiano wa kimapenzi na
mwanamke mwingine, lakini sikuwahi kufikiri kuwa anaweza kumgeuza binti
yake kuwa ¡®mke mwenza wangu¡¯,¡± anasema Mariam.
Kwa upande wake binti
aliyebakwa mwenye umri wa miaka tisa (jina tunalihifadhi), anakiri
kwamba baba yake huyo wa kufikia amekuwa akimfanyia vitendo hivyo mara
kwa mara, huku akimtisha kumchinja iwapo angetoa taarifa kwa mama yake
au mtu mwingine yeyote.
¡°Alikuwa akinifanyia mara kwa
mara, mama anapoondoka kwenda katika shughuli zake za biashara ya
mboga, alikuwa ananiita na kuniambia njoo ndani tufanye mambo na
kunikataza nisiseme nikisema atanichija,¡± anasimulia binti huyo.
Hija Ahmad ambaye ni
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Rahaleo, anasema alishtushwa na tukio hilo
ingawa juhudi za kumnasa mwanamume huyo hazijazaa matunda hadi sasa.
Ahmad anasema binti huyo kwa
umri alionao, anahitaji msaada wa matibabu ya kisaikolojia. ¡°Mtoto huyu
kwa sasa ameathirika kisaikolojia kutokana na kuzomewa na wenzake, mara
nyingi utamkuta amejitenga ¡-.nadhani unahitajika msaada wa kumtibu
kisaikolojia,¡± anasema.
Katibu wa asasi ya kutetea
haki za wanawake wilayani Newala (NEWORA), Mwanahamisi Fakihi
anathibitisha kupokea taarifa za tukio hilo na kwamba jitihada
zinaendelea kumsaka muhusika ili afikishwe mahakamani.
Ubakaji Newala
Mganga Mkuu wa Hospital ya
Wilaya ya Newala, Dk. Yudas Ndungile anasema matukio ya ubakaji
yameongezeka katika wilaya yao na takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2012
walipokea kesi saba za ubakaji na mwaka jana kesi 11.
¡°Matukio ya ubakaji ni hatari
kwa afya za wabakaji na wabakwaji, unajua kuna maradhi ya ngono ikiwa
pamoja na Ukimwi, pia watoto wanaobakwa husababishiwa madhara makubwa ya
kisaikolojia, wito wangu kwa jamii iamke kupambana na vitendo hivi vya
ubakaji,¡± anasema Dk. Ndungile.
Karani wa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Newala, Maweda Samuel anasema mwaka 2012 walipokea kesi saba za
ubakaji na kati ya hizo, kesi namba 134 ilivunja rekodi kwani washtakiwa
watatu walitiwa hatiani kwa kumbaka mwalimu na wote walihukumiwa kwenda
jela.
Samuel anasema kuwa mwaka jana
kulikuwa na kesi 11 za ubakaji mojawapo ikiwa ni ileinayomuhusu
mshtakiwa anayetuhumiwa kwamba alimlawiti mbuzi hadi kufa. Mshtakiwa
huyo yupo mahabusu hadi sasa kutokana na jamii kutaa kumwekea dhamana
kutokana na kuchukizwa na kitendo hicho.
Ofisa Ustawi wa Jamii wa
Wilaya ya Newala, George Martin anasema vitendo vya ubakaji kwa watoto
vinashamiri katika wilaya hiyo na kuhusisha na imani ya kishirikina kuhu
akieleleza kuwa tiba yake ni kutoa elimu kwa jamii juu ya athari za
vitendo hivyo.
¡°Kwanza jamii ishirikiane na
polisi katika kuwafichua wahalifu wa matukio haya ili sheria ifanye kazi
yake na kutoa fundisho kwa wengine,¡± anasema Martin.
Mkuu wa wilaya hiyo,
Christopher Magala anasema vitendo vya ubakaji havikubaliki ndani ya
jamii na kusisitiza kuwa watakaobainika kujihusisha na tabia hizo
watachukuliwa hatua za kisheria.
¡°Wananchi wasisubiri mambo
yaharibike ili tulaumiane, wahakikishe wanatoa taarifa hata kama ni za
siri polisi au mahala husika ili wabakaji wadhibitiwe,¡± anasema Magala.
Vitendo vya udhalilishaji wa
kijinsia ukiwamo ubakaji, vinaendelea kushamiri nchini licha ya kuwepo
kwa sheria ya makosa ya kujamiana ya 1998 (SOSPA) inayotoa adhabu ya
kifungo cha maisha jela au miaka isiyopungua 30 kwa mtu anayepatikana na
hatia kwa kosa hilo.
Tafiti zilizofanywa na Chama
cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) zinathibitisha kwamba
vitendo vya ukatili hususan ubakaji ni vingi katika jamii, chanzo kikuu
kikiwa ni kuporomoka kwa maadili na athari za utandawazi.
Chanzo: MWANANCHI
0 Response to " REHEMA: NILIMSHUHUDIA MUME WANGU JUMA AKIMBAKA MWANANGU WA MIAKA 9"
Post a Comment