Latest Updates

Aliyemshauri PNC aache muziki kwa kudai kuwa hajui kuimba ndiye aliyewekeza kwenye muziki wake



Mwimbaji toka Rock City Mwanza, PNC ameeleza kuwa moja kati ya vitu ambavyo hatavisahau ni pale alipojikuta akipewa sapoti ya hali na mali katika muziki na mtu ambaye awali alimshauri aachane na muziki kabisa kwa kuwa hajui kuimba.
PNC ameiambia tovuti  hii  kuwa mtu huyo ambayo hakutaka kumtaja jina alikuwa mtangazaji wa radio aliyemuona awali akiimba kwenye matamasha ya muziki jijini Mwanza, na PNC alipomfuata akiomba amsaidie alimpa ‘makavu live’ kuwa yeye sio muimbaji na ni bora aache muziki.
“Yaani huyo alishawahi kuniambia mimi ‘wewe hujui kuimba, inabidi tu kama vipi sio mpaka uimbe unaweza kufanya kazi nyingine. Tatizo mnalazimishalazimisha…mnadhani muziki ni mlaini eeeh.” Amesema PNC.
“Halafu mwisho wa siku sasa akaja kunikubali sana mpaka sasa akaja kusimamia zile project zangu zote, kiasi kwamba mimi mwenyewe natamani nije nimkumbushe unakumbuka ulishawahi kuniambia hivi na hivi.” Ameongeza.
Ameeleza kuwa wakati anaanza muziki alikuwa anaimba na rafiki yake anaitwa Raja Computer ambaye alikuwa anakubalika sana kwa watu lakini baadae akaamua kuokoka. Kupendwa kwa Raja Computer kulikuwa kunampa nguvu na matamanio zaidi ya kufanya vizuri lakini alikatishwa tamaa alipoambiwa aachane na muziki.
PNC amedai kuwa kauli ya mtu huyo awali ilimfanya anyong’onyee na kuacha kabisa kuwafuata tena watu wa media kuwaomba msaada na badala yake akaamua kwenda studio ambapo alipewa nafasi na producer Mo wa Mo Records enzi hizo na akarekodi wimbo aliouita ‘Mama’.
Baada ya wimbo huo kusikika hewani, mtu huyo alikuwa surprised na kudhani PNC wa kwanza alikuwa anaigiza tu ila alikuwa anajua kuimba zaidi ya alivyokuwa akimsikia.
“Nilivyotoa huo wimbo, yule meneja aliyekuwa ananisimamia kipindi kile akausikia akanambia ‘yaani wewe unajua kuimba hivyo! Au ulikuwa unavunga unaigiza wewe…Basi akanikubali sana na ndo tukaanza kufanya mipango.”
Ameeleza kuwa alimuita kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam na wakafanya kazi na kuisimamia albam yake ya kwanza

Related Post:

0 Response to "Aliyemshauri PNC aache muziki kwa kudai kuwa hajui kuimba ndiye aliyewekeza kwenye muziki wake"

Post a Comment