Latest Updates

Poll: Brazil wapendekeza mwanawake anaeacha wazi mwili wake anastahili kubakwa, wanawake wapinga kwa kupost picha

Kwa mujibu wa maoni ya raia wa Brazil waliofikiwa na timu ya utafiti iliyo chini ya taasisi ya serikali ya nchi hiyo (IPEA), raia wengi wa Brazil wamependekeza kuwa mwanamke anaeacha wazi mwili wake na kuonesha sehemu zilizostahili kufunikwa (kimaadili) anastahili kubakwa. Ripoti ya timu ya IPEA imetoa matokeo wiki hii ambayo yanaoesha kati ya watu 3,810 waliofikiwa na timu hiyo, watu 2,480 ambao ni asilimia 65 wameamua kuwa wanawake wanaojiweka watupu kwa lengo la kuonesha miili yao wanastahili kubakwa.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo asilimia 58.5 wameeleza kuwa kama wanawake wangejua jinsi ya kujitunza vizuri na kujiheshimu ingepunguza kwa kiasi kikubwa matukio ya ubakaji.
Hata hivyo matokeo hayo yamepokewa kwa hasira kubwa na wanawake wengi wa Brazil na baadhi ya wanaume ambao wamechukua maamuzi magumu.
Mwaandishi wa habari maarufu nchini Brazil, Nana Queiroz ameanzisha kampeni kwenye Facebook kupinga matokeo hayo na amewaalika wanawake wapige picha wakionesha vifua vyao wazi huku wakifunika sehemu ya matiti, kampeni ambayo imepewa jina ‘I don’t deserve to be raped’.
Brazil ni nchi ambayo inaongoza kwa starehe za ufukweni na wanawake warembo ambao hupenda kupiga picha ama kuonekana hadharani wakiwa wamevaa bikini au mavazi mengine ambayo yanaoenesha miili yao.
Wanawake wengi wanaoshiriki kucheza Samba kwenye maonesho mbalimbali huwa watupu ama nusu watupu.

0 Response to "Poll: Brazil wapendekeza mwanawake anaeacha wazi mwili wake anastahili kubakwa, wanawake wapinga kwa kupost picha"

Post a Comment