Latest Updates

Paul Okoye na mchumba wake Anita kufunga ndoa ya kitamaduni leo Nigeria, kuoneshwa Live kwenye TVMwanafamilia wa P-Square, Paul Okoye atafunga ndoa ya kitamaduni leo nchini Nigeria na mchumba wake wa muda mrefu Anita Isama.
Paul Okoye aliingia jana katika jiji lenye utajiri wa mafuta, Port Hartcourt ambapo ndoa hiyo itafungwa. Mwimbaji huyo aliwasiri akiwa na watu mbalimbali maarufu kama Kcee, mchekeshaji Agwu na muigizaji wa kike Suzan Peters.
Ndoa hiyo itarushwa moja kwa moja kwenye runinga kupitia HIP TV ambayo ni channel namba 324 kwenye DSTV.
Wanandoa hao watarajiwa wamekuwa katika uhusiano kwa muda wa miaka 10 na wiki iliyopita walitoa video kabla ya ndoa yao na kushare ujumbe ulioeleza hisia zao na kwa nini wameamua kufunga ndoa sasa.
“Tunafunga ndoa kwa sabubu sasa tuko tayari kwa ndoa kisaikolojia na kihisia. Alisema Anita na kuongeza kuwa anampenda Paul kwa sababu ni mwanaume asiyejivuna, na kwamba member huyo wa P-Square anampenda kwa kuwa alikuwa nae tangu mwanzo wa safari yake katika muziki.

0 Response to "Paul Okoye na mchumba wake Anita kufunga ndoa ya kitamaduni leo Nigeria, kuoneshwa Live kwenye TV"

Post a Comment