Kwa mujibu wa mtandao wa Abril Uno, uliomkariri Diana, alisema, “mimi ni shoga, na nashiriki vitendo vya ushoga, nimelijua hilo toka mdogo. Pia nimekuwa mkristo kwa maisha yangu yote, hivyo sitovumilia sharia yoyote inayopinga demokrasia katika taifa, ambayo italeta chuki kwa mtu yeyote sababu tu ya maumbile yake ya ngono”.
“sasa kwasababu nimeshajitangaza, niko tayari mbele ya sharia hii nione watakachofanya” Kamuntu aliongeza huku sauti ikikatikakatika hewani.
Mtangazaji wa redio hiyo, James Kasirivu alishindwa kujizuia kwa mshtuko na inaelekea hakuwa na la maneno ya kutamka kutokea kwenye kimywa chake. Muda wa kipindi hicho gafla ulipunguzwa na kuwekwa kwenye matangazo katika vipindi masaa machache baadae.
Katika kupinga masuala ya ushoga nchini Uganda, rais Yoweri Museven alitia saini muswada uliokamilika na kuwa sharia kamili ya kupinga vitendo vya ushoga jumatatu tarehe 24/02/2014 na kuhalalisha adhabu kali kwa watu wanaojihusisha na shughuli za ushoga, hatua ambayo inapingwa vikali nan chi mbalimbali duniani na kutishia mahusiano baina ya Uganda nan chi hizo ikiwemo Marekani.
Mtandao huo umeeleza katika taarifa yake kuwa, wakati taarifa hizi zinaandikwa, raisi Museveni pamoja na redio hiyo hawakuweza kupatikana kutoa maelezo yoyote kuhusiana na taarifa hiyo.
0 Response to "MTOTO WA MUSSEVENI AJITANGAZA 'SHOGA'"
Post a Comment