Latest Updates

CHRIS BROWN 'ATAPATAPA' KURUDIANA NA RIHANNA




Mwanamuziki maarufu nchini Marekani, Chris Brown inadaiwa kuwa ameachana na mpenzi wake wa sasa Karrauche na kuamua kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Rihanna.

Chris  ameripotiwa kumbwaga mpenzi wake Karrauche huku akidaiwa kutaka kurudiana na mpenzi wake wa zamani, Rihanna. 

Ripoti zinasema kuwa hii ilitokana na wivu ambao Chris ameshindwa kujizua kwa wasiwasi kuwa Rihanna sasa anarudiana na Drake ambaye ni adui yake mkubwa.

Mtandao wa Rada online umeripoti kwamba Chris alianza kumtumia Rihanna ujumbe wa simu kuanzia tarehe 20 februari, ambapo ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa na ndipo Karrauche alipoanza kuweka jumbe hizo katika mtandao wa Instagram na twitter, na kuacha kumfuata Rihanna katika mitandao ya kijamii.

0 Response to "CHRIS BROWN 'ATAPATAPA' KURUDIANA NA RIHANNA "

Post a Comment