MWANAMUZIKI kutoka Marekani Lil Wayne ameweka wazi msimamo wake wa
kuacha kurekodi tena albamu, huku akieleza kuwa albamu yake ya mwisho
itakuwa 'The Carter V'.
Alisistiza kuwa hiyo huenda ndio ikawa ni albamu yake kubwa ya mwisho
kama msanii, ingawa haikuwekwa wazi sababu za msanii huyo kueleza
kusimama kurekodi tena albamu.
Katika mahojiano na MTV, Lil Wayne alieleza kuwa hiyo ndio itakuwa
albamu ya mwisho kurekodi ingawa alidai kuwa atakaa muda mrefu bila ya
kufanya kazi ya kurekodi albamu nyingine.
Huku akiweka wazi kuwa endapo atatakiwa kurekodi albamu nyingine tena
atafanya hivyo lakini kwa kiasi cha dola 25,35 ikiwa ni moja ya
makubaliano yake na hao watakaotaka kufanya naye hiyo kazi.
Kauli hiyo si ya mara ya kwanza kusikia akisema kuacha kufanya kazi ya
muziki, ikumbukwe kuwa Wayne alishawahi kujitangaza kuacha kufanya kazi
hiyo June 2013.
0 Response to " LIL WAYNE KUSIMAMA KUFANYA MUZIKI?"
Post a Comment