Latest Updates

KIOJA MAHAKAMANI - 'RUKSA KUPIGA CHABO'

Mahakama moja imeatoa uamuzi kuwa kupiga picha watu za nguo za ndani kwa kupiga chabo (utaratibu unaojulikana kama “upskirting”) bila ridhaa ya mhusika sio kosa kisheria wakati akijibu swali muendesha mashtaka aliyetaka sheria hiyo iangaliwe upya.

Mchezo huo ni kama ule wa kupiga chabo kwa kuweka kioo chini alafu kuangalia msichana atakaesimama hapo bila kujua ili kuona nguo yake ya ndani.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na CNN leo, Mahakama Kuu ya Massachusett ilipitisha uamuzi huo jana(jumatano) kwamba sio kosa kumchungulia na kupiga picha nguo ya ndani ya mtu bila yeye kujua.

“abiria wa kike ambaye amevaa sketi au gauni au nguo nyingine kujisitiri sio sawa na mtu aliye “nusu uchi” bila kujali kilichopo au kisichopo chini ya sketi ikiwa kama nguo ya ndani au nguo nyingine” iliandikwa na Jaji Margot Botsford wa mahakama ya rufaa.

Mchambuzi wa sheria wa CNN, Sunny Hostin alisema kuwa sheria hiyo imepitwa na wakati kwani haiendani na teknolojia ya kisasa na kwamba ni udhalilishaji wa wanawake na faragha.

Uamuzi huo ulitokana na kesi inayomshtaki Michale Robertson, 32 aliyekamatwa mwaka 2010 akidaiwa kutumia simu yake ya mkononi kupiga picha na kurekoidi video wanawake

0 Response to "KIOJA MAHAKAMANI - 'RUKSA KUPIGA CHABO' "

Post a Comment