MKURUGENZI WA ITV NA RADIO ONE BI JOYSE MHAVILE AKIWA KATIKA MKUTANO HUO AMBAO ULIKUWA UNAFANYIKA NDANI YA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA TCRA JUU YA MUVIPA ONYO KALI VYOMBO HIVYO |
WAANDISHI WA HABARI KUTOKA VYOMBO MBALIMBALI WAKIWA WANASIKILIZA KWA MAKINI MKUTANO HUO |
MWENYEKITI WA KAMATI YA MAUDHUI KUTOKA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA TCRA AKIWASILISHA MAAMBUZI YA KAMATI HIYO JUU YA VITUO HIVYO VYA KURUSHA MATANGAZO MBELE YA WANAHABARI LEO |
Na Karoli Vinsent
MAMLAKA ya Mawasiliano nchini (TCRA) imevipa onyo kali
Itv na Startv pamoja na RadioFree,kutokana na kurusha Tangazo ambalo linakwenda
kinyume na Maadili,
Hayo,yalisemwa leo Jijini Dar es Salaam katika mkutano na Waandishi wa Habari na Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka
hiyo,Margaret Mnyagi ambapo alisema Kamati imefikia maamuzi hayo baada ya
kushauriana na Kamati Maudhui ya vipindi vya Runinga vya mamlaka hiyo.
“Tumefika maamuzi haya baada ya kukaa sisi kama kamati
ya Maudhui na kubaini tangazo la Policy Forum ambalo tangazo hilo linachochoe
watu wasilipekodi,Tangazo hilo
lilirushwa kwenye Runinga mbili ambazo ni Itv pamoja na Startv na redio ambayo
ni Radio Free”
“Napenda kuwatoa hofu wananchi kuwa atuchafanya
upendeleo wowote katika kutoa hukumu hii”alisema Mnyagi
Aidha Mamlaka hiyo imevitaka vyombo hivyo vilivyorusha
Tangazo hilo viwasilishe mwongozo wa urushaji wa Matangazo hayo,na pia Mamlaka hiyo imevionya vyombo hivyo
kutorudia kuonyesha Matangazo ya Uchochezi,na endapo watakaidfi Mamlaka hiyo
itawachukulia hatua kali za kisheria.
Kwa upande wake Meneja wa Mipango na Utafiti wa Sahara
media Nassani Lwehabula ambao ni wamiliki wa Startv,kissfm,Radio free,Gazeti
la Msanii wa Afrika alisema wao wamechukulia Hukumu hiyo ni kama Changamoto
kwao ya kufanya Vipindi vyao kwa umakini ili waweze kukuza maudhui yao,
Ikumbukwe Tangazo liloifanya Mamlaka ya Mawasiliano
nchini kuchukua Maamuzi hayo ni Tangazo la Taasisi isiyokuwa ya kiSerikali
inayojulika PolcyForum,ambapo katika Tangazo hilo linawahamasisha wananchi wasilipe kodi
mwenzi Januari Mwaka huu.
0 Response to "ITV,STAR TV NA RADIO FREE ZAPEWA ONYO KALI,NINI SABABU SOMA HAPA"
Post a Comment