Latest Updates

RIHANNA AJIPANGA KUGHARAMIA MAZISHI YA SHABIKI WAKE
MUIMBAJI wa muziki nchini Marekani Rihanna ameamua kugharamia mazishi ya shabiki wake mwenye umri wa miaka 14, kutoka nchini Brazil aliyeuwawa na baba yake wa kambo.

Uwamuzi huo wa kugharamia mazishi hayo umekuja mara baada ya shabiki huyo anayejulikana kwa jina la 'Thyago Fenty' anayedaiwa kuchomwa kisu hadi kufa na baba yake wa kambo aliyekuwa amelewa.

Ambapo katika tukio hilo baba huyo pia inadaiwa alimuua mdogo wake na mama yake mzazi katika tukio hilo hilo kwa kumchoma kisu hadi kupoteza maisha.

Baada ya muimbaji huyo kupata taarifa hiyo ya kuchomwa kisu kwa kwa shabiki wake huyo aliwasiliana na familia kwa ajili ya kutoa salaam zake za rambirambi pamoja na kugharamia mazishi yake.

Rihanna alitoa salamu za rambirambi kwa kupitia mtandao wa Twitter, huku akiahidi kugharimia shughuli nzima ya mazishi ya shabiki huyo.

0 Response to "RIHANNA AJIPANGA KUGHARAMIA MAZISHI YA SHABIKI WAKE"

Post a Comment