Latest Updates

ALICHO JIBU MASELE KUHUSU KUTUMIA UNGA                                         Crispian Masele
Mchekeshaji  mahiri Crispian Masele ‘Masele Chapombe’ anashutumiwa kwa utumiaji wa madawa ya kulevya na ulevi wa kupindukia hapo awali wapenzi wa filamu na vichekesho walikuwa wakiamini kuwa msanii huyo mwenye kipaji cha kuigiza ulevi alikuwa akiigiza tu na hatumii kilevi chochote, lakini sasa imebainika kuwa ni mlevi tena aliyekubuhu.

zinazomuandama akidai kuwa yeye ni mtu safi asiyetumia kilevi chochote na hausiki na madai hayo kwani yeye ni mtu anayejitambua na anajua madhara ya ulevi.

              Crispian masele

“Mimi hata siku moja sijawahi kutumia madawa ya kulevya, labda tu nahisi watu walikosa habari za kuandika, kwa sababu watu wanaonifahamu vizuri wanajua sina muda mchafu mimi nipo bize na kazi zangu,”

“Mambo mengine naona tu wenyewe, binadamu tunatofautiana kuna wengine hawanipendi hivyo wanaweza kunizulia lolote tu ili nafsi zao zifurahi, mara nyingi sitoki nyumbani nashinda hapo, sasa wananiona saa ngapi? Anasema Masele.
Hata hivyo msanii huyo akiwa jijini Tanga amekuwa akionekana au kuwa na urafiki na mateja huku akiwa katika hali ya ulevi, kwa sasa Masele yupo Dar.

0 Response to "ALICHO JIBU MASELE KUHUSU KUTUMIA UNGA"

Post a Comment