Latest Updates

PINDA APOKEA MISAADA YA WAATHIRIKA WA MAFURIKO WA MAGOL1(4)
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda, amepokea msaada ya mabati, mashuka, vyandarua na biskuti vyenye thamani ya sh. 141,045,000/- kutoka kwenye makampuni binafsi matatu na jumuiya za kidini mbili.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo leo Jumatatu Februari 3, 2014 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mwenyekiti wa Makampuni ya (MMI) Steel Ltd. Bw. Subhash Patel alieleza kuwa jumuiya yao imeguswa na tukio hilo na kuona umuhimu wa kutoa misaada hiyo.
Akikabidhi misaada hiyo, Bw. Patel alitoa wito kwa makampuni, taasisi za dini na watu binasi kuchangia waathirika wa mafuriko hayo ili waweze kuendelea na maisha yao ya kawaida.
Akipokea misaada hiyo, Waziri Mkuu Pinda alishukuru sana jitihada zilizooneshwa na kampuni hizo kwa misaada waliyotoa, kwani nyumba, Zahanati na makazi ya wananchi wengi yaliondoshwa na maji.
Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri Mkuu alisema: “Nilitembelea eneo lile na kuona kwa jinsi gani maji yalivyoathiri eneo kubwa kwa kuingia ndani ya makazi ya watu, hali iliyosababisha kupotea kwa mazao, chakula kingi kilipotea hivyo misaada bado inahitaji kwa wingi kwa wananchi wale”.
Waziri Mkuu alisema Rais ametoa maagizo kwamba Jeshi lijenge nyumba za muda ili kuweza kuwahifadhi wananchi wa eneo lile. “Serikali imefanya jitihada kwa kupeleka mahema, na kuanza ujenzi wa haraka wa daraja ili kurejesha usafiri katika hali ya kawaida.
Ametoa wito kwa wananchi na makampuni yanayotaka kuwasilisha misaada yao, wanaweza kuiwasilisha moja kwa moja kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na hapa Dar es Salaam wanaweza kuiwasilisha katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Maafa.

0 Response to "PINDA APOKEA MISAADA YA WAATHIRIKA WA MAFURIKO WA MAGOL"

Post a Comment