Latest Updates

LIL KIM NI 'MJAMZITO'HATIMAYE  Mwanamuziki Rapper kutoka nchini Marekani 'Lil Kim kwa mara ya kwanza amepata ujauzito wa mtoto wake wa kwanza.
Mwanamuziki huyo kwa mara ya kwanza ameuonesha ujauzito wake jana katika shughuri ya fashion week huko New York Marekani.
Mwanamama huyo mwenye umri wa miaka 39, jana ameonekana akiwa na hali hiyo ambapo alituma picha hizo kwenye ukurasa wake wa instagram, ambapo zilizua mijadala mbalimbali.
Picha hizo zilisambaa kwenye ukurasa wake, akionekana amekaa na Paris Hilton, ingawa hajaweka wazi juu ya ujauzito huo kama ni wa rapper mwenzake ambaye alikuwa na uhusiano naye wa kimapenzi anayeitwa Papers.

0 Response to "LIL KIM NI 'MJAMZITO' "

Post a Comment