KAMPUNI ya kutengeneza vinywaji baridi Tanzania Coca Cola, yazindua
kampeni ya 'Good Time ya Ukweli na Coca Cola' yenye lengo la kuwapa
fursa vijana kupata burudani ya muziki pamoja na michezo mbalimbali
itakayotoa fursa ya kushinda zawadi mbalimbali.
Kampeni hiyo itaambatana na kutoa burudani ya muziki kwa vijana katika
mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Arusha pamoja na
mjini Moshi kwa kuwatumia wanamuziki nyota wa hapa nchini.
Ambapo baadhi ya wanamuziki watakaotoa burudani hiyo kwa vijana ni
pamoja na Diamond Platanum, John Makini, Madee pamoja na Vanesa Mdee.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Saalam, Meneja wa
kinywaji hicho cha Coca Cola Tanzania, Maurice Njowoka alisema kuwa,
burudani hizo zitafunguliwa rasmi Februali 16 mwaka hii katika ufukwe wa
Coco Dar es Saalam ambapo msanii Diamond , Vanessa Mdee, Madee pamoja
na Joe Makini watafanya shoo.
"Lengo la burudani hizo ni kutoa fursa kwa vijana kufurahi pamoja na
marafiki huku wakiburudika na Coca Cola, ambapo burudani hiyo inatolewa
bure kwenye mikoa yote " alisema Njowoka.
Alieleza kuwa burudani hizo zitafanyika sehemu mbalimbali huku wakazi wa
Mwanza watafanya katika viwanja vya Furahisha, ambapo mkoani hapo
wanaume TMK, pamoja , Diamond pamoja na Madee watatumbuiza tamasha hilo
mkoani huko,
Ambapo alidai kuwa mfululizo wa burudani hiyo utazunguka katika miko
hiyo huku baaadhi ya wasanii hao wakiendelea kutoa burudani ya bure kwa
mashabiki wao
0 Response to "COCA COLA WAANDAA TAMASHA LA BURE"
Post a Comment