
Akizungumza kwa njia ya simu Ripota wa Mtandao huu, alisema kuwa, Viongozi hao wa Chadema, wamekamatwa na Polisi leo asubuhi na kuwashikilia kwa muda kituoni hapo wakihojiwa baada ya jana kupitisha muda katika mkutano wao waliofanya mkoani hapo.
Aidha imeelezwa kuwa viongozi hao walichelewa kufika eneo la mkutano baada ya Rubani wao kupotea angani na kufika eneo hilo zikiwa zimebaki dakika chache kabla ya muda wa mkutano kumalizika, jambo lililomfanya mwenyekiti huyo kuwaomba Polisi wasimamizi wa usalama kuongea japo kwa dakika chahe ili kuwajulisha wanachama wao kilichotokea.
DJ SEK
0 Response to "UPDATES::KUHUSU KUKAMATWA KWA MWENYEKITI WA CHADEMA,MH. MBOWE, MH. HALIMA MDEE NA MH. PETER MSIGWA NA JESHI LA POLISI MKOANI IRINGA"
Post a Comment