Latest Updates

TAZAMA PICHA JINSI ZITTO KABWE ALIVYOITEKA KASULU LEO NA KUFANYA MKUTANO MKUBWA

 Mbunge wa kigoma akiwa anasalimia wakazi wa kasulu leo,huku umati wa watu ukimfurahia
Mwami Zitto Ruyagwa Kabwe.... Kasulu baada ya kuvikwa cheo cha kimila
 Mamia  ya wakazi wa kasulu wakimlaki Zitto kabwe leo
 Zitto kabwe akisalimia wakazi wa kasulu waliojitokeza kumpokea leo
 Wakazi wa kasulu wakimsikiliza Zitto kabwe HAYA NI MANENO ALIYOPOST MH ZITTO KABWE MDA MFUPI ULIOPITA KATIKA AKAUNTI YAKE YA FACEBOOK
"Maisha ni mabadiliko; mabadiliko hayana ukomo; mabadiliko hayazuiliki kwa sababu bila mabadiliko hakuna ukuaji, bila mabadiliko hakuna maendeleo. Mabadiliko ni kiu kikubwa cha Tanzania kwa sababu mabadiliko huleta matumaini. Na kiu hii ni kubwa zaidi kwetu sisi vijana wa kizazi hiki kipya. Siasa za kizazi kipya cha viongozi ni siasa za majawabu ya kero za wananchi. Siasa za mabadiliko ni siasa za kujenga na kuimarisha; ni siasa za kuaminiana na kuheshimiana hata pale mnapopingana kimawazo. Ninataka tujenge siasa mpya Tanzania; siasa za mabadiliko; siasa zinazojenga matumaini ya kweli; siasa zinazowajali na kuwajengea uwezo wananchi wa Tanzania. Mungu ibariki Tanzania."

     By Dj Sek

0 Response to " TAZAMA PICHA JINSI ZITTO KABWE ALIVYOITEKA KASULU LEO NA KUFANYA MKUTANO MKUBWA "

Post a Comment