Latest Updates

Rais Dkt. Kikwete akutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa


D92A6952Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki Moon akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwenye ofisi yake iliyopo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani leo(24/12/2013).
D92A6977Bwana Ban Ki Moon alimwalika Rais Kikwete ambapo viongozi hao wawili walijadili masuala mbalimbali ya kimataifa hususan masuala ya amani na ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika kudumisha amani sehemu mbalimbali Afrika na katika nchi nyingine duniani. Tanzania ina majeshi ya kulinda amani katika nchi kadhaa ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Darfur nchini Sudan na Lebanon.
Rais Kikwete yupo jijini  New York nchini Marekani ambapo anaendelea vyema na ukaguzi wa kawaida wa afya yake.(picha na Freddy Maro)

0 Response to "Rais Dkt. Kikwete akutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa"

Post a Comment