Latest Updates

KWELI TANZANIA IMEBARIKIWA VIPAJI VYA HALI YA JUU MJUE MWANADADA "YUSTER NYAKACHARA"KUTOKA KATIKA KAMPUNI YA EAGLE ENTERTAINMENT AMBAYE AMEPANIA KUINUA FILAMU ZA KITANZANIA
Yuster Nyakachara ukilisikia jina hili kwa sasa unaweza ukajiuliza mara tatu tatu,Huyu ni Nani?na anatokea wapi?Basi Yuster Nyakaracha ni dada wa kitanzania mwenye malengo na anataka kuifikisha mbali sanaa yetu ya filamu za kitanzani.Kwa miaka takribani 10(kumi)mwanadada huyu amekuwa akizunguka dunia kwa ajili ya maonyesho mbalimbali ya sanaaa hasa ngoma za asili ya kitanzania.Kupitia sanaa hiii ya ngoma za asili kumemfanya kutembelea nchi zote za ukanda wa scandinavia ambazo ni sweden,finland,denmark,norway na zingine zote.Kutokana na safari hiyo ndefu ya takribani nchi kumi duniani ameweza kujifunza mambo mengi sana kuhusu sanaaa na ngoma na uigizaji,iliyompelekea kupata uzoefu wa kutosha katika sanaa ya filamu.
Kwa sasa mwanadada Yuster nyakachara amerudi nchini Tanzania na kuamua kufungua kampuni yake ya kutengeneza filamu aliyoipa jla la "EAGLE ENTERTAINMENT"kupitia kampuni hii mwanadada Yuster ni miongoni mwa watakaofanya vizuri sana kwenye sanaa ya soko la filamu za kitanzania.Hivyo basi mwanadada Yuster amewaomba wadau wote wa sanaa nchini Tanzania kushirikiana naye ili kuifikisha sanaa yetu mbali na hatimaye kufanikiwa kufahamika kimataifa kama wenzetu Ghana,Nigeri na zambia.Mtandao wetu ulipofanya mahojiano naye na kumuuliza je amejiandaaa vipi kukabiliana na soko la movie la Tanzania kwa kuwa kuna kampuni nyingi za kutengeneza movie?Yuster alijibu kwa umakini sana najua kuna makpuni mengi sana ya kutengeneza movie Tanzania lakini akasema yeye ameamua kuanzisha kampuni hii ya EAGLE ili kuleta ushindani katika utengenezaji wa filamu na hivyo kupelekea makapuni kutokulala kwa kujiamini wanaweza,Akaendelea kusema kuwa anajiamini kwa uzoefu wa takribani miaka 10 atafanya vizuri na kuweza kufanya mapinduzi katika sanaa ya Filamu za kitanzania,Hivyo basi tumpe sapoti mwanadada huyu ili aweze kuinua sanaa yetu.

1 Response to "KWELI TANZANIA IMEBARIKIWA VIPAJI VYA HALI YA JUU MJUE MWANADADA "YUSTER NYAKACHARA"KUTOKA KATIKA KAMPUNI YA EAGLE ENTERTAINMENT AMBAYE AMEPANIA KUINUA FILAMU ZA KITANZANIA"