Latest Updates

TIMBERLAND KUWASHIRIKISHA WAKONGWE WA MUZIKI
MTAYARISHAJI mkongwe wa muziki nchini Marekani Timberland ameuachia wimbo wake mpya unaojulikana kwa jina la 'Know Bout Me' ambao amewashirikisha wasanii wakongwe wa muziki huo akiwemo Jay Z pamoja na Drake.

Katika harakati za kutambulisha wimbo huo na kuufanya kuwa rasmi mwezi uliopita Timberland aliutambulisha wimbo huo katika ziara ya kimuziki ya msanii Jay Z 'Magna Carter' nchini Uingereza.

Kutokana na harakati hizo za mtayarishaji huyo mkongwe kuwashirikisha wasanii hao baadhi ya mashabiki wa wanamuziki hao walidai kuwa wimbo huo unaweza kuwa ni miongoni wa nyimbo zitakazofanya vizuri.


Hivi sasa Jay Z na Drake wanaendelea na ziara yao ya kimuziki ambapo Jay Z yupo katika ziara yake inayojulikana kwa jina la 'Magna Carter World Tour' barani Ulaya, huku Drake akiwa kwenye ziara yake nchini Marekani

0 Response to "TIMBERLAND KUWASHIRIKISHA WAKONGWE WA MUZIKI "

Post a Comment