Latest Updates

HUZUNI !!!! MSANII MAARUFU ALIA KAMA MTOTO


                              

Msanii maarufu wa sinema za Kibongo, Michael Sangu ‘Mike’ amepata pigo la kuondokewa na dada yake, Salma Said na kujikuta akilia kama mtoto mdogo na kusababisha watu kuwa na kazi ya ziada kumbembeleza.Mike alipatwa na pigo hilo wiki iliyopita baada ya dada yake huyo kuugua kwa muda mfupi akisumbuliwa na maumivu ya titi moja lililokuwa limevimba hali iliyosababisha kifo chake katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar.
“Naumia sana, dada yangu alikuwa kila kitu kwangu kwani alikuwa akinishauri mambo mbalimbali kuhusu maisha, ukweli ameniachia pengo kubwa sana ila ndiyo mipango ya Mungu nitafanyaje,” alilalama Mike kwa uchungu.

Mazishi ya dada huyo yalifanyika Ijumaa iliyopita katika Makaburi ya Kinondoni, Dar na kuhudhuriwa na watu kibao wakiwemo waigizaji wa filamu ambapo mkewe, Salome Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ alikuwa na kibarua kizito cha kumbembeleza Mike anyamaze.

0 Response to "HUZUNI !!!! MSANII MAARUFU ALIA KAMA MTOTO "

Post a Comment