Latest Updates

RAIS KIKWETE AMWAGIA SIFA YA NIDHAMU DIAMOND
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete, amewataka wasanii nchini kuwa na nidhamu katika kazi zao ili waweze kufikia malengo na mafanikio yao huku akimtolea mfano msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Nassibu Abdul 'Diamond Platnum' kuwa ni miongoni mwa wasanii wenye nidhamu nchini.
Aliyazungumza hayo hivi karibuni jijini Dar es Salaam katika kuitimisha semina ya fursa iliyoandaliwa na kituo cha Clouds Fm, ambapo semina hiyo ilizunguka zaidi ya mikoa 18 ikiwa na lengo la kuwafungua vijana kutambua fursa zinazowazunguka.
Kikwete alimpongeza msanii huyo nchini kuwa ni miongoni mwa wasanii wenye nidhamu ya kazi kutokana na thamani kujituma umakini na kufanya ubunifu kwenye kazi hiyo ambayo yeye ameichukulia kama ajila kwake.
Mbali na Diamond pia Rais alitoa mfano wa msanii wa Pop duniani Marehemu Michael Jackson kuwa ni miongoni mwa wasanii dunia aliyekuwa na nidhamu hali iliyopelekea kuwa na mafanikio makubwa kwenye kazi yake hiyo ya muziki.
"Diamond ni miongoni mwa wasanii nchini wenye nidhamu yeye ameufanya muziki kuwa ni ajira hivyo akili yake yote ameiweka kwenye muziki huo kuwa wakwanza kuanzisha kitu na kukuiendeleza, hivyo wasanii wanatakiwa kuwa na nidhamu ya kazi yao ilii waendelee kufanya vizuri" alisema Diamond.
Kwa upande wake msanii huyo aliweka wazi kuwa mafanikio yake yametokana na kujituma na kuwa na uthubuti wa kufanya jambo bila kuangalia mwingine atakavyolipokea.
"Nimekuwa nikithubutu kila siku bila kuogopa kukosea na kuwa na uwezo wa kusema nafanya na siyo nitafanya" aliweka wazi Diamond.

0 Response to "RAIS KIKWETE AMWAGIA SIFA YA NIDHAMU DIAMOND "

Post a Comment