Latest Updates

LULU ATEMBELEA OCEAN ROAD

Msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael 'Lulu' leo amefanya ziara ya kutembelea katika hospitali ya Ocean Road iliyopo jijini Dar es Salaam ambapo ameweza kutoa msaada wa fedha kwa ajili ya wagonjwa wa cancer hospitalini hapo. Lulu amebainisha hivyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika kuwa "Naamini mimi sio mwema sana hadi mungu akaniwezesha kuona mwezi huu nikiwa mzima mwenye afya kwa kutambua hilo nimeanza mwezi huu kwa kupita katika hospital ya Ocean Road na kutoa mchango ili kuwasaidia wagonjwa wa cancer, tuwe na utaratibu wa kuwakumbuka wahitaji kwa chochote tulichonacho"

0 Response to "LULU ATEMBELEA OCEAN ROAD"

Post a Comment