Latest Updates

LULU ALONGA NA BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Elizabeth Michael ‘Lulu’ambae ni msanii wa filamu Nchini, ameliomba Bunge kurekebisha sheria za Magereza katika vikao vyao vinavyoendelea mjini Dodoma.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam juzi, Lulu alisema kutokana na kukaa huko kwa mwaka mmoja, ameona mambo mengi ambayo yanatakiwa kufanyiwa marekebisho.

“Unaweza ukamkuta mfungwa ana miaka zaidi ya 20 lakini hajawahi kufikishwa mahakamani wala kuulizwa chochote kutokana na kitu ambacho kimempeleka hapo, kiukweli hata kama ana makosa haiwezekani kumkalisha miaka yote hiyo pasipo kusikilizwa,” alisema.

Alisema yeye amekaa huko kwa muda mfupi lakini amepata shida sana kuyazoea mazingira hayo, kwani huwezi kuishi kama nyumbani, hivyo ni vizuri ukiwekwa utaratibu mtu anasomewa kesi yake kwa muda gani.

Lulu alilazimika kukaa gerezani kwa muda huo kwa tuhuma za mauaji ya aliyekuwa nguli wa filamu nchini, Steven Kanumba, aliyefariki dunia nyumbani kwake Sinza Vatican Aprili 7, mwaka jana.
 
  by PRO24

0 Response to "LULU ALONGA NA BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA"

Post a Comment