Latest Updates

DR. MVUNGI AKIWA HOSPITALI BAADA YA KUVAMIWA NA MAJAMBAZI USIKU



MJUMBE wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini na mhadhiri mwandamzi wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Bagamayo (UB), Dk. Sengondo Adrian Mvungi, saa saba usiku wa kuamkia leo amevamiwa na watu wasiyojulikana nyumbani kwake Kibamba nje  kidogo ya jiji la Dar es Salaam na kumcharanga mapanga maeneo ya mwilini mwake ikiwemo sehemu za kichwani kwa madai kuwa watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walikuwa wakimshinikiza awapatie fedha na Dk Mvungi alipowaambia hana fedha ndipo walipoanza kumcharanga mapanga.

Mtoto mkubwa wa Dk. Mvungi aitwaye Dk. Natujwa Mvungi ameeleza kuwa baada ya watu hao kumjeruhi baba yake na kufanikiwa kuondoka, walimchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Tumbi mkoani Pwani ambapo amepatiwa huduma ya kwanza kisha kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo baadaye alipelekwa kwenye wodi katika Taasisi ya Mifupa (MOI) kwa ajili ya matibabu.
 
Dk. Mvungi aliwahi kugombea urais katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi.
 

0 Response to "DR. MVUNGI AKIWA HOSPITALI BAADA YA KUVAMIWA NA MAJAMBAZI USIKU"

Post a Comment