Latest Updates

Mambo 10 aliyoyasema Joseph Kusaga kwenye Power Breakfast

Kwenye Power Breakfast FEB20 Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Mr. Joseph Kusaga amesikika live kutoka Dubai, yako mengi kayazungumza, FIESTA2015, wasanii wa TZ, ishu ya dawa za kulevya, UCHAGUZI 2015 na story ya Clouds kuuzwa. Kwanza kuhusu mipango ya Clouds kusikika nchi nzima; “Kwanza nimshukuru sana mwenyezi MUNGU.. Kwa yale yote ambayo tuliyaomba na kuwekeza jitihada zetu yametimia, tulikuwa tumebakiza Nachingwea, Kasulu, Simiyu, Geita, Katavi na Njombe… Hiyo Mikoa tumeimilisha that means tumekamilisha kuipiga TANZANIA nzima kama tulivyoahidi mwaka jana“ “Sasa hivi tumejaribu kwa kiasi kikubwa sana kuona tunakwenda kwenye upande wa digital zaidi, kuingia kwenye mitandao.. tuna-launch Tanzania Box, Tanzania na dunia nzima watapata nafasi hiyo ya kuweza kuona the biggest OTT in Tanzania. Mtanzania yoyote leo ukiwa na nafasi ukiingia kwenye www.tanzaniabox.com utaona content yote ambayo iko humo ndani“ Fiesta 2015 ipo?; “FIESTA ni sherehe kubwa ya burudani.. Fiesta mwaka huu IPO.. iko palepale na tumeipanua zaidi kujaribu kunyanyua utamaduni wa KITANZANIA, vyakula vya kitanzania pamoja na kuipeleka kimataifa zaidi. Ilikuwa tuanze mwaka huu kutoka kwenda kwenye nchi nyingine lakini nafikiria tutaanza kutoka mwaka kesho.. FIESTA iko palepale na nafikiria itakuwa ni bora kuliko miaka yote FIESTA ya mwaka huu..“ Kingine ni kuhusu kufanya show nyingine kubwa ya kumleta msanii mkubwa mbali na Fiesta; “Tuko katika mazungumzo mazuri kidogo na wasanii wawili watatu ni mapema kuyazungumza, nafikiria kutakuwa na tamasha lingine zaidi ya ambalo litainvolve wasanii wakubwa.. Kuna tamasha lingine litakuja mapema sana pamoja na tamasha la utamaduni“ Dubai ni sehemu ambayo ina connection kubwa, hapa anazungumzia ishu ya kuwapeleka wasanii wa Watanzania; “Tuko katika mazungumzo na Diamond pamoja na wasanii wawili wadogo, tunachotaka kufanya ni kuhakikisha wasanii wa Tanzania wakubwa wanawabeba vilevile wasanii wadogo.. Diamond ni shahidi tuko katika mazungumzo ya mwisho ili aweze kuja na wasanii wengine either wa kati au wadogo ili waweze kuwapandisha na wale wadogo wapande..“ Kuhusu Uchaguzi Mkuu 2015; “Ni watanzania sisi wenyewe ndio wenyewe jukumu kubwa sana kwanza kujiandikisha kupiga kura and then kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anamchagua mtu ambaye kiukweli atampeleka kutoka kwenye level moja kwenda nyingine..“ Hapa anaongelea Clouds kuhusishwa na Chama chama cha CCM; “Nimeona kwenye mitandao, yamezungumzwa mengi kuhusu Clouds kuwa radio ya chama tawala CCM.. Mimi mwenyewe sina chama, niko neutral.. Kama kuna individual mmoja au wawili ambao ni mashabiki sio policy ya kampuni.. haturuhusu sisi. Freeman Mbowe ni rafiki yangu wa damu tunafahamiana miaka mingi zaidi ya miaka 30 kwa nini nisimpe nafasi yeye kama naendekeza chama“ Kumekuwa na ishu ya mauaji ya albino, hapa anaongelea hilo; “Nimeona juzi mtoto mdogo wametoa mikono, miguu nchi inakwenda wapi sasa? Watu wanafikiria maendeleo ni kuuana tena kwa vitu ambavyo havipo. Lazima nchi nzima sasa hivi tuseme kwamba hiyo kitu tunaipiga vita vibaya sana na nafikiria Hashtag inayosema #MimiNitakulinda ingeanza kutumika kwa Watanzania wote sasa hivi na kuhakikisha tunapigana vita kuokoa viumbe ambavyo kiukweli havina hatia“ Kesi ya dawa za kulevya na wasanii na vijana TZ; “Madawa ya kulevya ni kitu hatari sana.. imewaona watu wengi ambao nimewajua kwa muda mrefu wakiteketea.. Ukiingia umeingia kwenye shimo ambalo hutaweza kuokolewa.. hii vita inatakiwa ipiganiwe na kila mtu. Hawa watu wanaoharibu watoto wetu kwanini wasifuatiliwe? Tunakwenda kuchagua viongozi, lazima tuwe sober na tuwe clean kuanzia sasa mpaka tunapokwenda kuchagua.. #Tanzania2015NoDrugs. Wasanii wangeweza kuwa pamoja na kampeni hizi ingeweza sana kusaidia nchi yetu“ millardayo.com

0 Response to "Mambo 10 aliyoyasema Joseph Kusaga kwenye Power Breakfast "

Post a Comment