Latest Updates

MAKUNDI YANATUCHELEWESHA KUFIKIA KWENYE MAFANIKIO

RAIS wa Shirikisho la filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifwamba amedai kuwa wasanii na wadau wa filamu Bongo wanapaswa kubadilika na kuungana kwa ajili ya kuijenga tasnia ya filamu badala ya kujenga makundi yanayopinga bila sababu ya msingi.

“Majungu kuelekea katika uchaguzi yameshamiri, lakini si dhamira ya TAFF shirikisho limepanga kujenga misingi ya tasnia ya filamu, sasa tunashangaa watu wanashindwa kujipima kwa maendeleo, na kubuni ukurasa wa Facebook kwa ajili ya kuwatusi viongozi,”anasema Mwakifwamba.


“Kama unaona kuwa una sifa safi na hauna kashifa subiri muda ufike kasha gombea kuliko kuwachafua watu kwa njia mitandao na kuwapaka matope kama watu wasiofaa katika jamii,”

Mwakifwamba akifafanunua kuhusu hilo anasema kuwa kuna ukurasa ambao umetengenezwa kwa ajili ya kuwachafua viongozi waliopo madarakani huku watumiaji wa ukurasa huo wakijiita wakombozi wa filamu, wanachochea chuki na uhasama, lakini majina ya watu hao kapuni wanafahamika, na ameahidi kuita vyombo vya habari kuwaweka wazi.

0 Response to "MAKUNDI YANATUCHELEWESHA KUFIKIA KWENYE MAFANIKIO"

Post a Comment