Uganda Bill the African ameripoti kutoka kwenye bunge la nchi hiyo kwamba Wanaume kutoka kaskazini mwa Uganda wamefikisha maombi kwa Wabunge wao kuhusu ishu ya mipira ya kiume (Condom)
Hawa Wanaume wanataka Wabunge wao wawaambie wauzaji wa Condoms Uganda kupeleka saizi kubwa za Condom kutokana na zilizopo sokoni kutowatosha kwa sababu zina saizi ndogo na ndio maana hawazitumii.
Tom ambae ni Mbunge wa Moyo pamoja na Wabunge wenzake amesema >> ‘Nimeshuhudia hili kwamba watu wa maeneo hayo wanataka condom kubwa sababu wanauume mkubwa hivyo condom zilizopo ni ndogo na haziwatoshi kwenye uume….‘ Mbunge mwingine akasema ‘baadhi ya vijana wanalalamika kwamba baadhi ya condom wanazopewa ni fupi na haziwatoshi’
Serikali chini ya mashirika yake itabidi wafanye kazi ya kuongea na makampuni yenye tenda ya kupeleka condom Uganda ili yalete condom zinazowaenea Wananchi.
Vilevile mmoja wa Wabunge kwenye bunge hilo la Uganda amewapongeza Wabunge wenzake kwa sababu condom zinazowekwa kwenye vyoo vya bunge hilo vinavyotumiwa na Wabunge zimekua zikiisha mapema hivyo kuonyesha kwamba Wabunge hao ni watumiaji wazuri wa kinga hiyo.
Zaidi unaweza kuplay hapa chini kumsikiliza Bill…http://www.hulkshare.com/ytyuqtoegikg
0 Response to "Umeipata hii ishu ya Condom iliyotoka kwenye bunge la Uganda?"
Post a Comment