Rais wa zamani wa shirikisho la muziki/muziki wa injili nchini, Eddo November amepanga kuwaburuza mahakamani mwanamuziki Stara Thoma na Francis Kaswahili baada ya kumtuhumu kuiba fedha za mchango katika msiba wa mzee Gurumo.
Edo November ameweka wazi nia yake jana kupitia ukurasa wake wa facebook:
“....Najiandaa kuwapeleka Mahakamani Stara Thomas na Francis Kaswahili kwa Kuzusha juu ya Ulaji wa Kiasi cha Milioni Moja za Msiba wa Gurumo, Kama Mwanasheria naweza kuchafuliwa na Magazeti yakaripoti bila hata kujua ukweli kunihoji mie mlengwa je kwa asiye mwanasheria hali ipoje?
Ninacho waambia ndugu zangu kuwa bado nipo Madarakani mwisho wa wanapotosha Umma ni aibu kwao, ndugu zangu tutatoka washindi pamoja...!! Matatizo yalianza nilipomkemea Stara kwa kusema Injili hailipi hivyo ataimba Bongo Fleva kupata Chakula kisha atarudi kwenye Injili..Hii haikubaliki Popote Mie hata Kama Ni Rais wa Shirikisho la Muziki Bado nasimama kwenye nafasi kama Rais wa Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania, Injili lazima iheshimiwe na watu wote na kama haikulipi basi Umepotea njia, juzi nimemuandikia Ujumbe kuwa Mungu atabaki kuwa Mungu na. Visa vyake havitasimama wala havitakuwa sawa sawa na Isaiah 7:7 mzidi kuniombea Tutatoka washindi pamoja..Halleluya!”
0 Response to "Addo kuwashitaki Stara Thomas na Francis Kaswahili baada ya kumtuhumu kuiba fedha za msiba wa Gurumo"
Post a Comment