Latest Updates

Gucci Man ahukumiwa miezi 39 jela na kizuizi cha safari akitoka


Rapper Gucci Mane amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu na miezi mitatu jela kwa kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria.
Mahakama ilimkuta na hatia rapper huyo Mwezi May na alikuwa akisubiri hukumu ya kipindi atakachokaa jela. Tayari Gucci Mane ameshakaa rumande kwa kipindi cha miezi 11 kwa hiyo amebakiza miezi 28 katika kifungo hicho.
Mbali na kipindi hicho atakachokaa jela, jaji amemuwekea kizuizi cha kusafiri katika kipindi cha miaka mitatu baada ya kutoka jela na kulipa fine ya $5,000.
Ripoti ya polisi imeeleza kuwa marafiki wa Gucci Mane walipiga simu polisi September 14 mwaka huu kutoa taarifa kuwa rapper huyo amegeuka mbogo na anafanya uharifu mitaani.
Baada ya polisi kufika katika eneo hilo na kumkamata walimkuta na bunduki yenye risasi kinyume na sheria.

0 Response to "Gucci Man ahukumiwa miezi 39 jela na kizuizi cha safari akitoka"

Post a Comment