Latest Updates

'The Karate Kid 2' ya Jaden Smith na Jackie Chan yapata pigo

Filamu ya The Karate Kid iliyoigiwa na Jaden Smith na Jackie Chan imepata pigo baada ya muongozaji wa filamu hiyo kujitoa katika mradi huo.
Waandaaji wa filamu hiyo wameeleza kuwa muongozaji Breck  Eisner ametoka kwenye mradi wa filamu hiyo kutokana na mgongano/mgogoro wa ratiba. Filamu hiyo bado haijampata muongozaji mpya.
Hata hivyo filamu hiyo imeongeza waandishi wengine wawili kwenye timu yake, ambao ni Jeremiah Friedman na Nick Palmer.
Filamu ya kwanza ya The Karate Kid ya mwaka 2010 ilifanikiwa kufikia mauzo ya $343 millioni duniani kote.

0 Response to "'The Karate Kid 2' ya Jaden Smith na Jackie Chan yapata pigo"

Post a Comment