Latest Updates

STUDIO ZA NOIZ MAKAH KUGAWA MIXTAPE KWA WASANII WA HIP HOP


STUDIO za Noiz Makah chini ya Producer DX, zimetoa mixtape ya midundo ya hip hop 10 waliyoipa jina la Biashara Ngumu Volume 1, ambayo inagaiwa bure kwa msanii yoyote wa miondoko ya Hip Hop nchini.

DX alizungumza hayo katika moja ya mahojiano maalumu aliyoyafanya jijini Dar es Salaam,  kuwa jina la mixtape hiyo, ‘Biashara Ngumu’ linatokana na aina ya midundo iliyomo ambapo midundo mitano ni ya Hip Hop biashara (laini) na mitano mingine ni Hip Hop ngumu.

Alisema kuwa lengo la kuitoa  mixtape hiyo, ni kusaidia wasanii wachanga ambao wanandoto ya kufanya mambo makubwa kwenye muziki huu. 

“Nia ya projet yenyewe ni kuweza kusapoti wasanii especially wasanii chipukizi kwa sababu kwenye tasnia ya muziki especially category ya Hip Hop tuna wasanii wengi chipukizi wanataka kuonesha ujuzi wao kupitia talent shows, kupitia hizi open stage/open mic na hat offer wanazopewa katika studio mbalimbali hapa Tanzania. Sasa sisi kama Noiz Mekah tumeona ni vizuri kusapoti.”

Ameeleza kuwa beat hizo zitaendelea kutoka kama mixtape na hiyo ni Volume 1, kwa hiyo zinakuja nyingine zaidi na zinapatikana bure kupitia website ya mkito.com.

0 Response to "STUDIO ZA NOIZ MAKAH KUGAWA MIXTAPE KWA WASANII WA HIP HOP"

Post a Comment