Latest Updates

Nakaaya: Baada ya kupata mtoto amenipa nguvu ya kufanya muziki tena


Mwimbaji aliyefanya vizuri kwenye game na nyimbo kama Mr. Politician, Nakaaya Sumari amerudi tena kwenye game na kuachia wimbo mpya unaoitwa Blessing ambao amesema ni maalum kwa ajili ya mtoto wake.
Akiongea na Bongo Dot Home ya 100.5 Times Fm, Nakaaya ambaye aliwahi kushiriki mashidnano ya kuimba ya Tusker Project Fame, amesema kuwa alikuwa amekata tamaa na muziki lakini baada ya kumpata mwanae amepata nguvu ya kurudi tena kwenye game.
“Baada ya kumpata mwanangu imenipa changamoto na imenipa motisha ya kufanya muziki wangu tena. Kwa sababu kuna time ilifika nikawa nimeshindwa kufanya muziki tena nilikuwa sitamani tena kufanya muziki na nilikuwa nimeachana nao.” Amesema Nakaaya. #
Akifafanua kuhusu hilo amesema aliona kuwa ni bora afanye muziki wake ambao mwanae atakapokuwa na kuanza kuelewa atajivunia badala ya kusimuliwa kuwa mama yake alikuwa anafanya muziki.
Amesema tayari ameshakamilisha albam yake aliyoipa jina la Blessing na wanasubiri wakamilishe video na kisha waendelee kuachia wimbo mmoja mmoja.

0 Response to "Nakaaya: Baada ya kupata mtoto amenipa nguvu ya kufanya muziki tena"

Post a Comment