Latest Updates

JUSTIN BIEBER KUPANDISHWA KIZIMBANI


                            
Siku kadhaa baada ya Justin Bieber kubatizwa bafuni kwa rafiki yake na kutangaza kuanza maisha mapya, anatarajiwa kupanda kizimbani kujibu mashitaka ya kurusha mayai kwenye nyumba ya jirani yake, tukio alilolifanya January mwaka huu. 

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Mwanasheria wa serikali wa mji anaoishi Bieber ameeleza kuwa alipanga kufungua kesi ya uharibifu wa mali leo (June 16) dhidi ya Justin Bieber. 

Mapema January mwaka huu, jirani wa Justin Bieber aliripoti polisi tukio la Justin Bieber kurusha nyumbani kwake mayai kadhaa na kusababisha uharibibu uliokadiriwa kuwa wa thamani ya $20,000. 

Baada ya kuripoti tukio hilo, maafisa wa polisi walifika nyumbani kwa Bieber na kufanya upekuzi ampabo walimkamata rafiki yake aliyetajwa kwa jina la Lil Za, ambaye alikutwa na madawa ya kulevya aina ya Cocaine.

0 Response to "JUSTIN BIEBER KUPANDISHWA KIZIMBANI"

Post a Comment